MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alitarajiwa kuwasili England leo mchana kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kujiunga na Liverpool baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na wawakilishi wake.
Mpachika mabao huyo wa zamani wa Manchester City yuko karibu kusaini kikosi cha Brendan Rodgers na amekwenda huko kukamilisha dili hilo mara moja.
Baada ya kuwasili, Balotelli alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali ya klabu hiyo, Spire Liverpool kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo zaidi vya afya katika viwanja vya Melwood vinavyotumika kwa mazoezi na klabu hiyo.
Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo wa Italia hataweza kuichezea Liverpool dhidi ya klabu yake ya zamani, Manchester City Jumatatu usiku, katokana na muda wa usajili kwa leo kupita.
0 comments:
Post a Comment