• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 28, 2014

  MECHI ZA TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUCHEZWA TANGA, BUKOBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za Mgambo Shooting na African Sports za Tanga zitapambana Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) katika mechi ya majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kwa kiingilio cha sh. 1,000 tu.
  Mechi nyingine ya tiketi za elektroniki siku hiyo itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuzikutanisha timu za Kagera Sugar na Geita Gold SC ya mkoani Geita. Geita Gold iko Daraja la Kwanza.
  Kikosi cha Mgambo Shooting

  Kabla ya mechi hizo, Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) saa 3 asubuhi kwenye viwanja hivyo kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki pamoja na jinsi mfumo huo unavyofanya kazi.
  Washiriki wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa vituo vya Tanga na Bukoba, viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (KRFA) na Tanga (TRFA), makatibu na maofisa habari wa klabu za Kagera Sugar, Mgambo Shooting, African Sports na Geita Gold, mameneja wa viwanja vya Kaitaba na Mkwakwani na wasaidizi wao, maofisa usalama wa TRFA na KRFA, wachanaji tiketi, wasimamizi wa milangoni, wasaidizi (stewards) na waandishi wa habari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI ZA TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUCHEZWA TANGA, BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top