• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 30, 2014

  VAN GAAL 'AMPIGA SUB' DI MARIA MAN UNITED IKING'ANG'ANIWA NA WALIOTOKA DARAJA LA KWANZA

  KOCHA Louis Van Gaal leo ameiongoza Manchester United katika mchezo wa tatu mfululizo Ligi Kuu ya England bila kushinda, licha ya kumuanzisha mchezaji mpya, Angel de Maria aliyemsajili wiki hii kutoka Real Madrid kwa Pauni Milioni 59.7.
  United imetoka safe ya bila kufungana na timu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, Burnley Uwanja wa Turf Moor, hivyo ikikusanya pointi mbili katika tatu baada ya awali kufungwa 2-1 na Swansea Uwanja wa Old Trafford na kulazimishwa sare ya 1-1 na Sunderland Uwanja wa Light. 
  Angel di maria akipasua katikati ya wachezaji wa Burnley leo
  Di Maria akimpisha Anderson baada ya kushindwa kuifungia Man United
  Van Gaal alimpumzisha mchezaji huyo aliyeweka rekodi ya kusajiliwa kwa fedha nyingi zaidi kihistoria Uingereza dakika ya 70, nafasi yake akichukua Anderson. Aliwapumzisha pia Juan Mata dakika ya 87 akiingia Adnan Januzaj na Robin van Persie dakika ya 73 akiingia Dany Welbeck.  
  Kikosi cha Man United kilikuwa; De Gea, Jones, Evans, Blackett, Young, Fletcher, Di Maria/Anderson dk70, Mata/Januzaj dk87, Valencia, Rooney na Van Persie/Welbeck dk73.
  Burnley; Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Arfield, Jones, Marney, Taylor/Reid dk88, Ings/Barnes, dk78 na Jutkiewicz.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VAN GAAL 'AMPIGA SUB' DI MARIA MAN UNITED IKING'ANG'ANIWA NA WALIOTOKA DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top