• HABARI MPYA

  Wednesday, August 27, 2014

  MOROCCO YAIKACHA STARS MCHEZO WA FIFA, SASA KUKIPIGA NA BURUNDI BUJUMBURA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MOROCCO imechomoa kucheza na Tanzania katika kalenda ya FIFA na sasa Taifa Stars itacheza na Burundi Septemba 5, mwaka huu mjini Bujumbura.
  Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa amesema Morocco imejitoa kwa sababu imesema haitaweza kuwapata wachezaji wake wa kimataifa.
  Mwesigwa amesema sasa Taifa Stars itacheza na Burundi mjini Bujumbura siku hiyo hiyo. Kocha Mholanzi, Mart Nooij, tayari ameita kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mchezo huo.

  Hao ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
  Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
  Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio 9ZESCO, Zambia).
  Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOROCCO YAIKACHA STARS MCHEZO WA FIFA, SASA KUKIPIGA NA BURUNDI BUJUMBURA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top