• HABARI MPYA

    Monday, August 18, 2014

    MAN CITY YAANZA NA MOTO WAKE LIGI KUU ENGLAND

    MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wameanza vizuri harakati za kutetea taji lao, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Newcastle United, Uwanja wa St. James Park.
    Katika mchezo huo uliotanguliwa na maombelezo ya Liam Sweeney na John Alder, waliofariki kwenye ajali ya ndege ya MH17, City ilipata bao moja kila kipindi. 
    David Silva amefunga Manchester City ikianza vizuri mbio za kutetea taji

    Alianza kiungo David Silva dakika ya 39, kabla ya mshambuliaji Sergio ‘Kun’ Aguero kupiga la kuhakikisha ushindi dakika ya 90- siku chache baada ya nyota hao wote kusaini mikataba mipya na timu hiyo ya Etihad.
    Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Clichy, Kompany, Dimichelis, Kolarov, Toure, Fernando, Nasri/Milner dk77, Jovetic/Fernandinho dk72, Silva na Dzeko/Aguero dk81.
    Newcastle United; Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Anita/Obertan dk62, Gouffran/Aarons dk73, Colback, Sissoko, Cabella na Riviere/Perez dk80.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY YAANZA NA MOTO WAKE LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top