Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI
KIUNGO wa zamani wa Yanga SC, Stephen Bengo ametokea benchi na kuipa KCC ya Uganda ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi B, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, jioni ya leo Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda.
Bengo aliingia dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Owen Kasuule na akaenda kufunga bao hilo pekee dakika ya 70 kwa mpira wa adhabu, baada ya Brian Umony kuangushwa umbali wa mita 30.

Mshindi: Stephen Bengo ameifungia bao pekee la ushindi KCC ikiiua 1-0 APR, ambayo sasa itakutana na Rayon katika Robo Fainali Jumanne
KCC sasa inamaliza kileleni mwa Kundi B, kwa pointi zake tisa, mbele ya APR yenye pointi saba na Atletico ya Burundi pointi sita, zote zinakwenda Robo Fainali, wakati Telecom ya Djibouti na Gor Mahia ya Kenya zinaaga.
Kwa matokeo ya leo, mechi za Robo Fainali Jumanne zitakuwa kati ya Polisi ya Rwanda na Atleitco, Rayon na APR zote za Rwanda, wakati Jumatano Azam itamenyana na El Merreikh ya Sudan na KCC na Atlabara ya Sudan Kusini.
0 comments:
Post a Comment