• HABARI MPYA

    Sunday, July 13, 2014

    PSG YATAKA KUIPOKONYA TONGE MDOMOMI MAN UNITED, DI MARIA HUENDA AKATUA UFARANSA

    KLABU ya Paris Saint-Germain ipo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumpata winga wa Real Madrid, Angel Di Maria, ambaye pia anatakiwa na Manchester United. 
    Mshambuliaji huyo wa pembeni wa Argentina mustakabali wake haueleweki Bernabeu baada ya Real kuwa katika mpango wa kumsajili nyota wa Colombia, James Rodriguez. 
    Pamoja na hayo, kocha Carlo Ancelotti hayuko tayari kumpoteza Di Maria, ambaye alikuwa na mchango mkubwa msimu uliopita wakati Real ikitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa Rais Florentino Perez amemtambulisha Rodriguez kama 'galactic mpya'.
    Yuko juu: Di Maria alikuwa ana msimu mzuri uliopita Real Madrid na sasa yuko njiani kuondoka

    PSG sasa wanaamini wanaongoza mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, Di Maria, ambaye ana miaka minne katika Mkataba wake ya kuwa kazini Madrid. 
    Real inaweza kusikiliza ofa ya kuanzia Pauni Milioni 50 kumuuza Di Maria owe kutoka kutoka PSG na United.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PSG YATAKA KUIPOKONYA TONGE MDOMOMI MAN UNITED, DI MARIA HUENDA AKATUA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top