• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 30, 2014

  MAN UNITED YAPIGWA BAO NA LAZIO SAINI YA BEKI KISIKI LA UHOLANZI LINALOPIGA HADI MABAO

  KLABU ya Lazio imetangaza kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Uholanzi, Stefan de Vrij kutoka Feyenoord ambaye alikuwa kwenye rada za Manchester United.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliichezea mechi zote saba Uholanzi ikimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil, na alifunga bao lake la kwanza Oranje katika ushindi wa kukumbukwa wa 5-1 hatua ya makundi dhidi ya Hispania.
  Taarifa kwenye akaunti ya Tweeter ya Lazio imesema leo kwamba; "Lazio inaweza kuthibitisha kusajiliwa kwa Stefan de Vrij kutoka Feyenoord,".
  Kisiki: Stefan de Vrij akiwa na Medali yake ya mshindi wa tat wa Kombe la Dunia baada ya Uholanzi kuifunga Brazil 3-0 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAPIGWA BAO NA LAZIO SAINI YA BEKI KISIKI LA UHOLANZI LINALOPIGA HADI MABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top