• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 24, 2014

  XAVI WA HAITI ATUA AZAM FC NA KUFANYA MAMBO ADIMU

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Haiti, Peterson Joseph maarufun kama Xavi wa Haiti ametua Azam FC kwa majaribio na katika siku yake ya kwanza leo alikuwa kivutio.
  Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog alimuanzisha Xavi huyo wa Haiti katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting na kuoyesha uwezo mkubwa wa kuiongoza timu kwenye safu hiyo.
  Meneja wa Azam FC, Jemadari Saidi Kazumari ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kwamba na Peterson, wachezaji wengine waliokuja majaribio ni beki Mghana Ben Achaw aliyekuwa anacheza Thailand na kiungo mshambuliaji, Serge Lofo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Peterson Joseph ndani ya Azam FC

  Omog akasema baada ya mechi alikuwa anahitaji kiungo mzoefu na hapana shaka kwa uwezo aliounyesha mchezaji huyo anadhani anaweza kuwa amepata jibu la tatizo lake.
  Peterson Joseph aliyezaliwa Aprili 24 mwaka 1990 kwa sasa anachezea Sporting Kansas City ya Ligi Kuu ya Marekani, ambayo jana ilifungwa mabao 4-1 na Manchester City katika mchezo wa kirafiki.
  Awali alicheza Aigle Noir AC ya Ligi Kuu uya Haiti kabla ya kuhamia SC Braga ya Ureno Januari mwaka 2009 kabla ya kupelekwa kwa mkopo FC Vizela ya Daraja la Pili.
  Joseph aliyejiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Marekani, Sporting Kansas City Septemba 1, mwaka 2011, aliichezea kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya Haiti katuka mechi ya kuwania klucheza Fainali za Olimpiki dhidi ya Bahamas.
  Peterson akiwa na Lionel Saint- Preux, mchezaji mwingine wa Haiti ambaye tayari amesajiliwa Azam FC 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: XAVI WA HAITI ATUA AZAM FC NA KUFANYA MAMBO ADIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top