• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  ASHANTI YATUPWA NJE KOMBE LA ROLLINGSTON

  ASHANTI United imetupwa nje ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Rollingston baada ya kufungwa bao 1-0 na Twalipo, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika bila bao na ilibaki moja tu kutimia dakika 30 za nyongeza mchezo uhamie kwenye penalti kuamua mshindi, lakini Suleiman Bofu akamaliza kazi.
  Godfrey Joachim wa Twalipo akimtoka beki wa Ashanti jioni hii Chamazi

  Mshambuliaji huyo hatari alimalizia shambulizi la kushitukiza kuipatia bao lililoipeleka fainali Twalipo.
  Twalipo sasa itamenyana na mshindi kati ya Azam FC na EMIMA ya Tabata, mchezo ambao unaendelea hivi sasa Chamazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ASHANTI YATUPWA NJE KOMBE LA ROLLINGSTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top