• HABARI MPYA

    Monday, July 14, 2014

    NI UJERUMANI BINGWA KOMBE LA DUNIA 2014

    NI Ujerumani. Ujerumani imetwaa ubingwa wa dunia, baada ya kuiangusha Argentina kwa bao 1-0 katika mchezo wa Fainali Uwanja wa Maracana mjini Rio de Jeneiro, Brazil.  
    Shukrani wake, Mario Gotze aliyeingia kuchukua nafasi ya Miroslav Klose dakika 88, aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 112.
    Hilo linakuwa taji la nne la Kombe la Dunia kwa Ujerumani na sifa zimuendee kipa Manuel Neuer aliyeokoa mabao mengi ya wazi na kuwakatili Argentina walioongozwa na nyota wao, Lionel Messi.
    Ujerumani wakishangilia na Kombe la baada ya mechi
    Shujaa; Mario Gotze akifunga bao la ubingwa
    Mario Gotze akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi kwa Ujerumani

    Refa Nicola Rizzoli wa Italia alikataa bao la Gonzalo Higuain dakika ya 32 akimalizia krosi ya Lavezzi, kwa kuwa mchezaji huyo aliotea, ingawa tayari alikwishaanza kushangilia.
    Kikosi cha Ujerumani kilikuwa; Neuer, Lahm, Boateng, Hummels, Howedes, Kramer/Schurrle dk32, Schweinsteiger, Muller, Kroos, Ozil, Klose/Gotze dk88.
    Argentina: Romero, Zabaleta, Demichelis, Garay, Rojo, Biglia, Mascherano, Perez/Gago dk86, Higuain/Palacio dk78, Messi na Lavezzi/Aguero dk46.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI UJERUMANI BINGWA KOMBE LA DUNIA 2014 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top