• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 21, 2014

  PIGO MAN CITY, NEGREDO AVUNJIKA MGUU NA ATAKUWA NJE MIEZI MITATU

  MSHAMBULIAJI Alvaro Negredo atakuwa nje ya Uwanja kwa miezi mitatu baada ya kuumia kikanyagio cha mguu wa kuli katika mchezo wa kirafiki baina ya Manchester City na Hearts. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amethibitisha taarifa za kuumia kwake kwa kuposti picha ya mguu wake ukiwa umefungwa kizuio, lakini amesema atarajea akiwa ana nguvu kuliko alivyowahi kuwa daima.
  "Nataka ujue kwamba itakuwa ngumu kwa miezi michache ijayo," ameposti. "Nimevunjika mguu na nitakuwa nje kwa miezi michache. Nitarudi mwenye nguvu kuliko daima,".

  Nje: Mshambuliaji wa Manchester City, Alvaro Negredo atakuwa nje kwa miezi mitatu baada ya kikanyagio kuvunjika mguu
  In a boot: Negredo posted this image of his foot as he confirmed the injury
  Mguu wa Negredo alivyouposti kuthibitisha kuumia kwake

  Mshambuliaji huyo wa Hispania hivi karibuni amekuwa akihusishwa na taarifa za kurejea nyumbani kwao kujiunga na Atletico Madrid, baada ya kuona mambo hayamuendei sawa kaskazini mwa England.
  Pamoja na hayo, mchezaji huyo anayekwenda kwa jina la utani 'The Beast' amesema anafurahia City na hana mpango wa kuwahama mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PIGO MAN CITY, NEGREDO AVUNJIKA MGUU NA ATAKUWA NJE MIEZI MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top