• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  LOIC REMY AFELI VIPIMO VYA AFYA, DILI LA KUTUA LIVERPOOL LAFA KIFO CHA KAWAIDA

  MPANGO wa Loic Remy kutua Liverpool kwa dau la Pauni Milioni 8.5 umekwama baada ya mchezaji huyo kufeli vipimo vya afya Marekani.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikwenda  Boston mapema wiki hii baada ya Liverpool kufika bei yake na yeye mwenyewe kukubali vipengele vya mkataba wake binafsi na klabu hiyo kabla ya kufanyiwa vipimo vya afya.
  Hata hivyo, suala la vipimo vya afya yake lilichukua muda mrefu kuliko kawaida, na majibu yalipotoka, Liverpool ikaamua kuachana naye. 
  Ikia tayari imekwishamuuza Luis Suarez kwenda Barcelona, Liverpool italazimika kuamua ama kutafuta mshambuliaji mwingine wa kucheza pamoja na Daniel Sturridge na Rickie Lambert au kubaki na hao hao kwanza.
  Amekwama kutua Liverpool: Loic Remy alikaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda kwa Wekundu wa Anfield, lakini vipimo vya afya vimemuangusha
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LOIC REMY AFELI VIPIMO VYA AFYA, DILI LA KUTUA LIVERPOOL LAFA KIFO CHA KAWAIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top