• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 25, 2014

  HATIMAYE MOURINHO AMREJESHA DROGBA CHELSEA

  MKONGWE Didier Drogba ametimiza ndoto zake za kurejea Chelsea.
  Nyota huyo wa Ivory Coast amesaini Mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge, na kuwa gwiji wa klabu hiyo baada ya awali kusajiliwa na Jose Mourinho kwa Pauni Milioni 24 mwaka 2004. Na Drogba amesema asingeweza kukataa fursa ya kufanya kazi na Mreno huyo tena.
  "Ulikuwa ni uamuzi rahisi - Nisingekataa fursa ya kufanya kazi na Jose tena. Kila mmoja anafahamu uhusiano maalum nilionao na klabu hii na wakati wote nahisi kama nyumbani kwangu.

  Amerudi: Drogba amerejea Chelsea baada ya miaka miwili tangu aondoke
  Dotted line: The Ivorian striker completes his medical and puts pen to paper on a new one-year deal
  Kushoto anapima afya na kulia anasaini mkataba wa mwaka mmoja

  Kwa upande wake, Mourinho amesema hana wasiwasi Drogba ataisaidia Chelsea, kwa sababu bado anaamini ni mmoja wa washambuliaji duniani.

  "Anakuja kwa sababu ni mmoja wa washambuliaji bora Ulaya. Nafahamu haiba yake vizuri sana na nafahamu kama akirudi hatalindwa na historia au kile alichokifanya katika klabu hii mwanzo," amesema Mourinho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HATIMAYE MOURINHO AMREJESHA DROGBA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top