• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 22, 2014

  RODRIGUEZ AANGUKA MIAKA SITA REAL MADRID BAADA YA KUMFUNIKA RONALDO KOMBE LA DUNIA

  KLABU ya Real Madrid imekubali kumsajili mfungaji bora wa Kombe la Dunia, James Rodriguez kutoka Monaco kwa mkataba wa miaka sita.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Colombia amekubali kusaini mkataba wa miaka sita Madrid baada ya kufuzu vipimo vya afya leo. Atatambulishwa jioni ya leo.
  Hakuna ofa iliyothibitishwa na klabu hiyo kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini taarifa zinasema Madrid imelipa kiasi cha Pauni Milioni 60, ambazo zinamfanya Rodriguez awe mchezaji mamba tatu ghali duniani kihistoria baada ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.

  Tayari kutambulishwa: Rodriguez anatua Madrid baada ya kumfunika Cristiano Ronaldo katika Kombe la Dunia
  Signed, sealed and delivered: Real Madrid welcome James Rodriguez with a picture from his medical
  Real Madrid imeposti picha hii kumkaribisha James Rodriguez baada ya kufuzu vipimo vya afya
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RODRIGUEZ AANGUKA MIAKA SITA REAL MADRID BAADA YA KUMFUNIKA RONALDO KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top