• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 29, 2014

  RONALDO AREJEA REAL MADRID, LAKINI AJIFUA PEKE YAKE KIVYAKE

  MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo jana ameungana na wachezaji wenzake wa Real Madrid katika mazoezi ya kujiandaa na msimu nchini Marekani. 
  Ilikuwa ni siku yake ya kwanza anafanya tena mazoezi na timu yake hiyo, baada ya kufanya vibaya kwenye Kombe la Dunia akiwa na nchi yake, Ureno iliyotolewa katika hatua ya makundi akiambulia kufunga bao moja tu.
  Alilakiwa na mania ya mashabiki katika uwanja wao wa mazoezi mjini Los Angeles kabla ya kwenda kufanya mazoezi mepesi peke yake, huku wenzake wakiendelea na program kamili.
  Amerudi: Cristiano Ronaldo amerudi mazoezini Real Madrid kujiandaa na msimu mpyaLone runner: He most trained by himself as he looked to recover his fitness
  Ronaldo akikimbia peke yake kujiweka fitiBack in action: Fabio Coentrao and Sergio Ramos are among those to have also returned
  Fabio Coentrao na Sergio Ramos pamoja na wachezaji wengine wa Madrid wakijifua tofauti na Ronaldo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AREJEA REAL MADRID, LAKINI AJIFUA PEKE YAKE KIVYAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top