• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  REAL MADRID YACHAPWA NA INTER MILAN KWA MATUTA

  REAL Madrid imefungwa kwa penalti 3-2 na Inter Milan katika michuano ya Kombe la Kimataifa jana, kufuatia sare ya 1-1 mjini California, Marekani.
  Nyota wa Wales, Gareth Bale alitangulia kuifungia Real Madrid dakika ya 10 kabla ya Samir Handanovic kuisawazishia Inter Uwanja wa California Memorial.
  Katika mikwaju ya penalti, wachezaji wawili wa Real, Isco na Asier Illarramendi mikwaju yao iliokolewa na kipa Juan Pablo Carrizo kabla ya kinda Omar Mascarell kupaisha.
  Inter itakutana na Manchester United mjini Washington Jumanne, wakati Madrid itamenyana na Roma mjini Dallas siku hiyo hiyo. 
  Heshima: Kinda Raul de Tomas (kushoto) akimpongeza Bale baada ya kuifungia Real bao la kwanza katika mechi za kujiandaa na msimu
  Hero: Goalkeeper Juan Pablo Carrizo (centre) is congratulated by his team-mates after saving two penalties
  Shujaa: Kipa Juan Pablo Carrizo (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kuokoa penalti mbili
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID YACHAPWA NA INTER MILAN KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top