• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 28, 2014

  AZAM BINGWA KOMBE LA ROLLINGSTON 2014

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Rollingston baada ya kuichapa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ya Mgulani Twalipo bao 2-0 katika fainali jioni hii Uwanja wa karume, Dar es Salaam. Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ aliyefunga bao la kwanza dakika ya tatu, baada ya kuwatoka vizuri beki wa kulia wa Twalipo, Ally Mbonde na beki wa kati Ally Athumani kisha kumtungua kipa wao, Kulwa Baumba.
  Jamil Balotelli kushoto akimiliki mpira pembeni ya mabeki wa Twalipo leo Uwanja wa Karume

  Beki wa Twalipo akimpunguza kasi winga wa Azam FC, Farid Mussa
  Twalipo ilipoteza mwelekeo mapema tu baada ya bao hilo, na wachezaji wake kuanza kucheza rafu nyingi, badala ya kutengeneza mipangop ya kusawazisha bao.
  Azam walitumia mwanya huo kucheza mpira wa kuachiana pasi za haraka uwanjani kuwakwepa ‘wapiga kiatu’ wa jeshini na kufanikiwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa wanaongoza 1-0.  
  Kikosi cha Azam FC leo 
  Jamil Balotelli akimtoka mtu 
  Wachezaji wa Champion na Bom Bom wakionyeshana kazi 


  Kipindi cha pili, mchezo ulizidi kunoga, Twalipo wakisaka bao la kusawazisha na Azam wakitafuta mabao zaidi- hali iliyosababisha mashambulizi ya pande zote mbili.
  Alikuwa ni Adam Omar Soba aliyeihakikishia Kombe la kwanza la Rollingston Azam FC baada ya kufunga bao la pili dakika ya 88.
  Katika mchezo wa kwanza wa kuwsaka mshindi wa tatu, Champion ya Kawe ilitwaa ubingwa wa U17 kwa kuifunga 1-0 Bom Bom ya Ilala kwenye Uwanja huo huo, Karume.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM BINGWA KOMBE LA ROLLINGSTON 2014 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top