• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  LEWANDOWSKI APIGA BONGE LA BAO BAYERN MUNICH

  MCHEZAJI mpya wa Bayern Munich, Robert Lewandowski jana ameendelea kung'ara katika timu yake mpya baada ya kufunga bao zuri katika safe ya 2-2 na Borussia Monchengladbach mchezo wa kujiandaa na msimu.
  Mshambuliaji huyo wa Poland aliyetua kama mchezaji huru kutoka wapinzani wao wa Bundesliga, Borussia Dortmund -tayari amefunga mabao mawili tangu awasili.
  Bao la pili ni la jana alipomtungua kipa mbele ya mabeki wake wanne ndani ya boksi.
  Bao tamu: Robert Lewandowski akipitisha mpira juu ya mabeki na kipa wao kufunga bao zuri
  Happy days: Lewandowski gets the congratulations from Franck Ribery on his Bayern return
  Siku za furaha: Lewandowski akipongezwa na mwenzake Franck Ribery aliyerejea Bayern baada ya kupona

  Na baada ya Bayern kutoa safe ya 2-2 mchezo ulihamia kwenye mikwaju ya penalti, ambako walishinda, na ilikuwa ni furaha mno kwa Franck Ribery aliyerejea uwanjani baada ya kupona maumivu yaliyomfanya akose fainali za Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LEWANDOWSKI APIGA BONGE LA BAO BAYERN MUNICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top