• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  MANJI AREKEBISHA KAMATI YA UTENDAJI YANGA SC, AMUINGIZA TARIMBA AWAMWAGWA KIBAO

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
  Yussuf Manji kulia na makamu wake, Clement Sanga

  1. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Sports Club (YANGA) kwa mamlaka waliyopewa na Wanachama,kubadilisha, kupunguza au kuongeza Mjumbe yeyote kwenye Kamati ya Utendaji wakati wowote,kulingana na changamoto wanazoziona zinazoikabili Klabu ya YANGA, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kutoa taarifa rasmi, kuwa Kamati ya Utendaji ya YANGA na Kamati zote ambazo ziko chini ya Kamati ya Utendaji zitavunjwa kuanzia tarehe 31 Julai, 2014.

  2. NVile vile, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya YANGA kwa juhudi zao za kutekeleza shughuli za Klabu.

  3. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Klabu ya YANGA Bw.Yusuf Manji na naibu wake Bw.Clement Sanga wanatangaza Kamati ya Utendaji mpya ya Young Africans Sports Club ambayo itakuwa madarakani kuanzia 1 Agosti, 2014 kama inavyoelezwa na kila Mjumbe anavyotajwa hapo chini anakuwa na majukumu ya msingi ya kusimamia kama inavyoonyeshwa pembeni ya jina lake.

  WAJUMBE WAPYA WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA NI HAWA WAFUATAO:

  1.Bw.Abubakar Rajabu - Mradi wa Jangwani City

  2.Bw.Sam Mapande - Sheria na Utawala Bora

  3.Bw.George Fumbuka - Uundwaji wa Shirika

  4.Bw.Waziri Barnabas - Vibali vya Hatimiliki na Mahusiano na Wafadhili

  5.Bw.Abbas Tarimba - Mipango na Uratibu

  6.Bw.Isaac Chanji na Bw.Seif Ahmed - Uendelezaji wa Mchezo

  7.Bw.Musa Katabalo - Mauzo ya Bidhaa

  8.Bw.Mohammed Bhinda - Ustawishaji wa Matawi

  9.Bw.David Ndeketela Sekione - Uongezaji wa Wanachama

  10.Bw.Mohammed Nyenge - Utangazaji wa Habari, Taarifa, Matangazo n.k.

  WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ILIYOUNDWA UPYA WATASIMAMIA KIMSINGI KAMATI NDOGO ZIFUATAZO:

  •Kamati ya Maadili - Bw.Sam Mapande
  •Kamati ya Nidhamu - Bw.Sam Mapande
  •Kamati ya Uchaguzi - Bw. Sam Mapande
  •Kamati ya Uchumi na  Fedha - Bw.George Fumbuka na Bw.Waziri Barnabas
  •Kamati ya Mashindano - Bw.Seif Ahmed & Bw.Isaac Chanji
  •Kamati ya Soka la Vijana na Wanawake - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
  •Kamati ya Ufundi - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji

  5. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanamategemeo makubwa kuwa waliotajwa hapo juu watahakikisha wana timiza malengo yaliyokusudiwa na YANGA ili“DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO” mpaka hapo itakapoamuliwa kubadilishwa au kutenguliwa vinginevyo.

  6. Mwisho,tunawaomba ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha kuwa YANGA inapiga hatua mbele na inafanikiwa katika kufikia malengo na mipango yake ya maendeleo ya muda mfupi na ya muda mrefu kwa manufaa ya Klabu, Timu na wana YANGA popote walipo duniani.
  “MUNGU AIBARIKI YANGA.”
  (BENO NJOVU)
  KATIBU MKUU- YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANJI AREKEBISHA KAMATI YA UTENDAJI YANGA SC, AMUINGIZA TARIMBA AWAMWAGWA KIBAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top