• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 26, 2014

  ETO'O AIFUNGIA MABAO MAWILI BARCELONA DHIDI YA PORTO KATIKA MCHEZO WA KUMUAGA DECO

  VIKOSI viwili vilivyoshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa awamu tofauti jana viliungana kuichezea Barcelona katika mechi dhidi ya FC Porto, kumuaga kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Deco.
  Mchezo huo uliowahusisha wachezaji nyota kama Lionel Messi, Eidur Gudjohnsen, Benni McCarthy na Paulo Ferreira, ulimalizika kwa sare ya 4-4, huku Samuel Eto'o akifunga mabao mawili na Deco aliyechezea nusu moja kila timu, akiifungia bao moja kila timu, likiwemo la mwisho la Porto lililoamua matokeo.
  Mabao ya Porto yalifungwa na Derlei dakika ya tatu, McCarthy dakika ya 15, Jankauskas dakika ya 62 na Deco dakika ya 89, wakati ya Barca yalifungwa na Eto'o dakika za 54 na 68, Deco 57 na Messi 81.
  Kikosi cha Porto kilikuwa: Baia, Ferreira, Costa, Emanuel, Valente, Costinha, Maniche, Mendes, Deco/Jankauskas dk46, Derlei na McCarthy.
  Barcelona: Jorquera, Oleguer, Belletti, Gerard, Sylvinho, Davids, Van Bommel, Van Bronckhorst, Giuly/Deco dk46, Ezquerro/Eto'0 dk46 na Gudjohnsen/Messi dk46.
  Messi na Deco wakimpongeza Eto'o baada ya kufunga
  Magwiji: Samuel Eto'o na Deco wakisalimiana Uwanja wa Estadio de Dragao mjini Porto kabla ya mchezo
  A familiar sight: Messi streaks past two defenders who end up on the floor trying and failing to take the ball off the Barcelona maestro on his first game after the World Cup
  Messi akiwatoka mabeki wa Poro
  Still got it: Former Blackburn and Porto striker Benni McCarthy vies for the ball with former Barcelona defenders Sylvinho and Oleguer
  Benni McCarthy akipambana katikati ya Sylvinho na Oleguer
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETO'O AIFUNGIA MABAO MAWILI BARCELONA DHIDI YA PORTO KATIKA MCHEZO WA KUMUAGA DECO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top