• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 22, 2014

  STARS NA MAMBAS ZAINGIZA MILIONI 158, KIKOSI CHARUDI KAMBINI TUKUYU

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.
  Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sh. 74,432,095.
  Mechi ya Taifa Stars na Msumbiji imeingiza Sh Milioni 158

  Tunawashukuru washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
  Wakati huo huo: Kikosi cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji.
  Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS NA MAMBAS ZAINGIZA MILIONI 158, KIKOSI CHARUDI KAMBINI TUKUYU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top