• HABARI MPYA

    Monday, July 21, 2014

    ARSENAL YAFIKA BEI KIPA LA COLOMBIA KOMBE LA DUNIA

    KLABU ya Arsenal imekubali kutoa Pauni Milioni 3.2 kwa ajili ya kumnunua kipa wa Nice, David Ospina. 
    Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 aling'ara na Colombia wakati wa Kombe la Dunia na anatarajiwa kumpa changamoto Wojciech Szczesny. Ospina amekataa ofa ya Valencia.
    Ospina alikuwa mmoja wa makipa waliokuwa kivutio kikubwa katika Kombe la Dunia, hakiiwezesha Colombia kufika Robo Fainali, ambako ilitolewa na wenyeji Brazil.
    Anatakiwa: Kipa wa Columbia katika Kombe la Dunia
    Wakati huo huo; Arsenal, inamtaka pia kiungo wa Sporting Lisbon mwenye thamani ya Pauni Milioni 35, William Carvalho.
    Tayari Arsenal imemsajili mshambuliaji nyota wa Chile,A lexis Sanchez kutoka Barcelona
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAFIKA BEI KIPA LA COLOMBIA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top