• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  LOGARUSIC AICHAMBUA SIMBA B NA KUSEMA; “MCHEZAJI MMOJA TU PALE”

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic amesema kwamba katika timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya klabu hiyo, ameona mchezaji mmoja tu anayefaaa kwa kikosi chake cha kwanza.
  Logarusic aliyasema hayo jana Uwanja wa Karume, Dar es Salaam baada ya Simba B kutolewa na Azam FC katika Robo Fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, Rollingston kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90.
  Loga katikati akiwa na Kocha Msaidizi, Suleiman Matola kulia na Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Said Tuliy kushoto 

  “Nimeona mchezaji mmoja tu,”alisema Logarusic alipoulizwa kuhusu Simba B, ameona vipaji vingapi kwa ajili ya kikosi cha kwanza baadaye.
  “Simba ni timu kubwa, lazima mchezaji aonyeshe uwezo sana kudhihirisha yuko tayari kucheza timu kubwa kama hii,”aliongeza.
  Hata hivyo, Logarusic hakuwa tayari kumtaja mchezaji aliyemvutia kutoka kikosi hicho kwa kuhofia kuwakatisha tamaa wengine. “Wanatakiwa wajibidiishe sana kufikia kiwango cha kuchezea Simba SC, kwa sasa bado sana,”aliongeza. 
  Lakini katika kikosi cha Simba B kilichoishia Robo Fainali ya michuano ya Rollingston, kuna wachezaji watatu waliosajiliwa kwa ajili ya timu ya wakubwa- ambao ni Peter Manyika, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Ibrahim Hajibu.   
  Maneno ya Loga ni ujumbe wa wazi kwao- kwamba wanakabiliwa na changamoto ya kupandisha uwezo wao kama wanataka kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Wekundu hao wa Msimbazi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LOGARUSIC AICHAMBUA SIMBA B NA KUSEMA; “MCHEZAJI MMOJA TU PALE” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top