• HABARI MPYA

    Friday, July 18, 2014

    SERENGETI BOYS YAIKOSAKOSA AMAJIMBOS, KOCHA ATAMBA KWENDA KUWAMALIZIA KWAOA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imelazimishwa sare ya bila kufungana na Afrika Kusini, Amajimbos katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Matokeo hayo yanamaanisha, Serengeti Boys itahitaji sare ya mabao katika mchezo wa ugenini, au kushinda kabisa ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo katika kuwania tiketi ya Fainali zitakazopigwa Niger mwakani.
    Amajimbos waliuanza mchezo vizuri wakilitia kwenye misukosuko lango la Serengeti kwa dakika takriban 20 za mwanzo, lakini taratibu mchezo ulianza kubadilika na wenyeji wakageuza kibao.
    Athanas Mdamu wa Serengeti Boys kushoto akijaribu kumtoka Notha Ngcobo wa Amajimbos

    Serengeti ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga kipindi cha kwanza na nafasi nyingine mbili zaidi za wazi pia za kufunga kipindi cha pili, ambacho watoto wa nyumbani walitawala zaidi mchezo.    
    Kocha wa Serengeti, Hababuu Ali alisema kwamba vijana wake waliuanza mchezo kwa kuelemewa kutokana na woga wa kucheza mbele ya umati wa mashabiki kwa mara ya kwanza. “Lakini walipozoea hali, wakatulia na kuanza vizuri,” amesema Hababuu.
    Kuhusu wapinzani wao, Hababuu amesema kwamba Amajimbos si wazuri kiufundi zaidi wana nguvu na kasi na kwa sababu hiyo ana matumaini ya kupata matokeo mazuri ugenini.
    Kikosi cha Serengeti Boys; Mitacha Mnacha, Abdallah Jumanne/Mashaka Ngujiro dk23, Issa Baky, Adolph Mutasingwa/Kelvin Farrel dk10, Martin Kiggi, Omar Wayne, Athanas Mdam, Ali Mabuyu, Abdul Bitebo/Mohamed Mussa dk86, Prosper Mushi na Baraka Yussuf.
    Amajimbos; Mondili Mpoto, Nelson Maluleke, Simon Nqoi, Notha Ngcobo, Keanu Cupido, Tendo Mukumela, Katlego Mohamme, Athenkosi Dlala, Sibongankonke Mbatha/Felix Noge, Luvuyo Mkatshana/Vuyo Mantjie na Khanyiso Nayo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAIKOSAKOSA AMAJIMBOS, KOCHA ATAMBA KWENDA KUWAMALIZIA KWAOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top