• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 31, 2014

  PAUL SCHOLES AMPA USHAURI WA BURE VAN GAAL MAN UNITED; "SAJILI MABEKI, SAFU YA ULINZI KIMEO BABA"

  GWIJI wa Manchester United, Paul Scholes amemuagiza kocha Louis van Gaal kununua mabeki wawili kwa kuwa kuna udhaifu kwenye safu ya ulinzi.
  Labda enzi za utawala wao zimepita, lakini wakati United inawatema Nemanja Vidic, Rio Ferdinand na Patrice Evra msimu huu, imepoteza wachezaji watatu ambao wameshinda mataji 16 ya Ligi Kuu ya England baina yao.
  Kupoteza aina ya uzoefu huo ni pigo kwenye klabu, kwa mujibu wa Scholes, ambaye anafikiri Van Gaal anapaswa kusajili mabeki wapya wawili wa kati. 
  Kazini: Chris Smalling, akipambana na Mauro Icardi, sasa ndite tegemeo la United beki ya kati
  Bwana mkubwa: Louis van Gaal anahitaji kununua mabeki wapya wawili, ushauri wa gwiji wa United, Scholes

  "Ana mabeki watatu wa halisi wa kati. Michael Keane na Tyler Blackett wanakuja vizuri, lakini kwa kuwa hawana uzoefu, anakosa kitu muhimu baada ya kuwapoteza Rio, Vidic ma Evra.
  "Phil Jones, Chris Smalling na Jonny Evans wote ni mabeki wazuri, lakini wan a matatizo ya majeruhi. Natumai wangeongeza watu, ili kuweza kuhimili vishindo vya msimu.
  "Nina uhakika watafanya vizuri, lakini nafikiri angetazama mabeki kadhaa wa kuongeza kikosini,". amesema’ 
  Wakongwe wameondoka: United itawakosa mabeki watatun wakongwe kama Nemanja Vidic na Rio Ferdinand, anayeichezea timu yake mpya QPR pichani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PAUL SCHOLES AMPA USHAURI WA BURE VAN GAAL MAN UNITED; "SAJILI MABEKI, SAFU YA ULINZI KIMEO BABA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top