• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 28, 2014

  DEJAN LOVEN ATUA LIVERPOOL KWA DAU LA REKODI TANGU TIMU IANZISHWE

  BEKI wa kimataifa wa Croatia, Dejan Lovren amekamilisha uhamisho wake kutua Liverpool kwa dau la Pauni 20 kutoka Southampton.
  Sasa mchezaji huyo anaweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na Wekundu hao wa Anfield akipiku dau la Pauni Milioni 18.6, ambalo Liverpool ililipa kumsajili beki wa Paris St Germain, Mamadou Sakho Septemba mwaka jana.
  Lovren, ambaye amekuwa mlengwa chaguo la kwanza la beki wa kati katika mawindo ya kocha Brendan Rodgers dirisha hili la usajili, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu vipimo vya afya Merseyside.

  Sasa ni mwekundu wa Anfield: Lovren akiwa ameshika jezi ya Liverpool viwanja vya mazoezi vya timu hiyo, Melwood 
  On the move: Dejan Loven has sealed a £20m switch to Liverpool from Southampton
  Dejan Loven ametua kwa dau la Pauni Milioni 20 kutoka Southampton
  Warrior: Lovren becomes the most expensive defender in Liverpool's history
  Lovren sasa ni beki ghali zaidi kihistoria kuwahi kutokea Liverpool 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DEJAN LOVEN ATUA LIVERPOOL KWA DAU LA REKODI TANGU TIMU IANZISHWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top