• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 22, 2014

  DUNGA KOCHA MPYA BRAZIL, ASEMA AMEFURAHI ILE MBAYA

  SHIRIKISHO la Soka Brazil (CBC) limeteua Dunga kuwa kocha mpya wa timu ya taifa leo, wiki mbili baada ya kipigo cha ainu cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia, kilichomfanya kocha Luiz Felipe Scolari abwage manyanga.
  Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50, aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Brazil kilichotwaa Kombe la nne la Dunia mwaka 1994, mara ya mwisho alikuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2010 alipofukuzwa baada ya timu kutolewa katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia Afrika Kusini.
  "Nina furaha kurejea,"aliwaambia Waandishi wa Habari.

  Dunga amerejeshwa kuinoa Brazil baada ya kuboronga Kombe la Dunia chini ya Scolari 
  Headache: Scolari resigned after the World Cup where Brazil were thrashed 7-1 by Germany in the semis
  Scolari alijiuzulu baada ya Brazil kufungwa 7-1 na Ujerumani Kombe la Dunia

  Aliiongoza Brazil hadi Robo Fainali ilipotolewa kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Uholanzi, lakini akalaumiwa kwa mbinu zake mbovu na kufukuzwa na nafasi yake kuchukua Mano Menezes.
  Awali aliiwezesha timu hiyo kushinda mechi 42, ndani take akitwaa mataji ya Copa America mwaka 2007 na Kombe la Mabara mwaka 2009, akipoteza mechi sita tu kati 60. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DUNGA KOCHA MPYA BRAZIL, ASEMA AMEFURAHI ILE MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top