• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 24, 2014

  LAMPARD ATAMBULISHWA RASMI NEW YORK CITY FC

  KIUNGO Frank Lampard amekamilisha uhamisho wake klabu ya New York City FC ya Ligi Kuu ya Marekani, maarufu MLS na kutambulishwa leo. 
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 ameondoka Chelsea mwishoni mwa msimu baada ya kuichezea kwa misimu 13 akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa klabu hiyo kwa mabao yake 211.
  Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa New York City FC na wa pili mwenye nina kubwa, baada ya David Villa kutoka Atletico Madrid.

  Karibu Marekani: Frank Lampard ametambulishwa rasmi leo New York City FC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LAMPARD ATAMBULISHWA RASMI NEW YORK CITY FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top