• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 22, 2014

  BEKI BINGWA LA DUNIA KUTUA MAN UNITED, VAN GAAL AENDEA MBIO SAINI YAKE

  BEKI Mats Hummels yuko mbioni kujiunga na Manchester United wiki hii akitokea Borussia Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 16, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
  Klabu hizo mbili bado hazijafanya mazungumzo kwa ajili ya uhamisho huo, lakini timu ya Old Trafford inajiamini mno inaweza kumpata beki huyo hodari.
  Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25 aling'ara kwenye Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani iliyoibuka bingwa nchini Brazil, kiasi cha kumvutia hadi kocha mpya wa United, Louis van Gaal.
  Bingwa: Mats Hummels alitoa mchango mkubwa Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia, na sasa anataka kuhamishia mafanikio yake Man United
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI BINGWA LA DUNIA KUTUA MAN UNITED, VAN GAAL AENDEA MBIO SAINI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top