• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 26, 2014

  PIGO LIVERPOOL, ADAM LALLANA AUMIA GOTI NA ATAKUWA NJE WIKI SITA

  MATUMAINI ya Adam Lallana kuanza kwa kishindo Liverpool yamepata pigo baada ya kuumia goti ambalo litamfanya awe  nje ya Uwanja kwa wiki sita.
  Kiungo huyo wa England, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na Liverpool kwa siku nne baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 23.6 kutoka Southampton, atakosa mechi tatu za kwanza za Ligi Kuu ya England — ukiwemo mchezo wa nyumbani dhidi ya klabu yake ya zamani na mechi za ugenini dhidi ya Manchester City na Tottenham.
  Na pia anaweza kukosa mchezo wa ufunguzi wa kufuzu Euro 2016 dhidi ya Uswisi Septemba 8 ugenini. Lallana aliumia mazoezini Alhamisi na wasiwasi wa Liverpool umeongezeka baada ya majibu ya vipimo alivyofanyiwa. 
  Pigo kubwa: Brendan Rodgers atamkosa mchezaji mpya, Adam Lallana mwanzoni mwa msimu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PIGO LIVERPOOL, ADAM LALLANA AUMIA GOTI NA ATAKUWA NJE WIKI SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top