• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 29, 2014

  HATIMAYE LIVERPOOL YASAJILI STRAIKA MKENYA

  KLABU ya Liverpool imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye asili ya Kenya, Divock Origi ingawa kinda huyo wa miaka 19 atabaki katika klabu yake Lille ya Ufaransa kuochezea kwa mkopo msimu ujao.
  Kinda huyo alikuwa kivutio kwenye Kombe la Dunia ingawa alikuwa kwenye dada za Wekundu hao kabla ya hao waliokuwa wakimfuatilia tangu akichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15.
  Origi amesafiri kwenda kujiunga na kikosi cha Liverpool Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya baada ya kukamilisha usajii wake.

  Amesajiliwa: Liverpool imekamilisha usajili wa Divock Origi

  "Nina furaha sana sana, na ninajivunia kujiunga na klabu hii kubwa kama Liverpool kuonyesha nia na mimi. Nimevutiwa sana,"amesema na kunukuliwa na tovuti ya klabu hiyo.
  "Kwangu, imekuwa ni kutimia kwa ndoto kuchezea klabu kubwa. Nafahamu Liverpool ni klabu yenye historia kubwa, hivyo kwangu ilikuwa sahihi.
  "Wakati wote nimekuwa naangalia Liverpool kwenye TV wakati nilipokuwa mdogo na unapoona wachezaji kama Gerrard na Sturridge, inakuvutia kufahamu kwamba unakwenda kucheza nao,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HATIMAYE LIVERPOOL YASAJILI STRAIKA MKENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top