• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 22, 2014

  USAJILI LIGI KUU TFF YAONGEZA WIKI MBILI TIMU KUMALIZA MAMBO

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa wiki mbili ili kuzipa klabu nafasi ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa. Hivyo hatua ya kwanza ya usajili inakamilika Agosti 17 mwaka huu badala ya Agosti 3 ya awali.
  Kutokana na marekebisho hayo, kipindi cha uhamisho kinakamilika Agosti 17 mwaka huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu.
  Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1 na 2 mwaka huu.
  TFF imesogeza mbele muda wa usajili kwa wiki mbili

  Uhamisho wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za usajili unatakiwa uwe umekamilika kufikia Septemba 7 mwaka huu. Uthibitisho wa hatua ya mwisho ya usajili utafanywa Septemba 15 mwaka huu.
  Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015 itaanza Septemba 20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: USAJILI LIGI KUU TFF YAONGEZA WIKI MBILI TIMU KUMALIZA MAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top