• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 28, 2014

  MAN CITY YAIFUMUA AC MILAN 5-1

  MANCHESTER City imeitandika mabao 5-1 AC Milan katika mchezo wa kujiandaa na msimu mjini Pittsburhg usiku wa kuamkia leo, huku mshambuliaji Stevan Jovetic akifunga mabao mawili dakika za 12 na 58.
  Mabao mengine ya City yalifungwa na Sinclair dakika ya 14, Navas dakika ya 23 na Iheanacho dakika ya 26, wakati bao pekee la Milan lilifungwa na Sulley Muntari dakika ya 43.
  Mchezo huo ulichelewa kuanza kwa dakika 30 kipindi cha pili kutokana na mvua kubwa ya mawe kunyesha uwanjani.
  Kikosi cha Man City kilikuwa; Clichy; Boyata/Rekik dk77, Nastasic, Kolarov/Richards dk70, Navas/Leigh dk77, Fernando/Garcia dk62, Zuculini/Rodwell 77, Sinclair; Jovetic/Guidetti dk70 na Iheanacho/Huws dk62.
  AC Milan; Agazzi; De Sciglio/Albertazzi dk68, Rami/Mexes dk68, Alex/Bonera dk46, Constant/Abate dk46, Poli/Essien dk46, Cristante, Muntari/Saponara dk68; Honda/Pinato dk86, Niang/Mastour dk87 na El Shaarawy/Balotelli dk 46.

  Mtaalamu: Kiungo wa AC Milan, Sulley Muntari akitafuta ya kumchokoka Jesus Navas wa Man City
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIFUMUA AC MILAN 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top