• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 30, 2014

  BABA YAKE TEVEZ AACHIWA BAADA YA SAA NANE ZA KUSHIKILIWA NA WATEKAJI

  BABA wa mchezaji wa zamani wa Manchester United na Manchester City, Carlos Tevez aliyetekwa jana nchini Argentina, ameachiwa baada ya saa nane za kushikiliwa. 
  La Nacion ya Argentina imeripoti kwamba Juan Carlos Cabrera alikuwa anaendesha gari lake katika Manispaa ya Moron, jimbo la Buenos Aires, wakati anatekwa asubuhi ya leo.
  Klabu ya Tevez, Juventus ilithibitisha kumruhusu mshambuliaji huyo kwenda Argentina baada ya tukio hilo asubuhi ya jana.
  Sasa shwari; Carlos Tevez alilazimika kurejea Argentina kumuokoa baba yake aliyetekwa
  Carlos Tevez akiwa na baba yake, Juan Carlos Cabrera 

  Gari aina ya Volkswagen Vento ilikutwa imetekelezwa na tovuti za  Argentina zikaripoti kwamba watekaji walikuwa wanataka fedha ili kumuachia. Hata hivyo, baada ya hapo suala hilo lilifanywa kuwa siri kwa matakwa ya familia ya Tevez.
  Tevez alichukuliwa na shangazi yake mjamzito na mumewe, Segundo Tevez akiwa mdogo na kuanza kulelea tangu hapo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BABA YAKE TEVEZ AACHIWA BAADA YA SAA NANE ZA KUSHIKILIWA NA WATEKAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top