• HABARI MPYA

    Monday, July 21, 2014

    KUMEKUCHA ZIARA YA REAL MADRID NCHINI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KUMEKUCHA. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kuhusu ziara ya kikosi cha wachezaji nyota waliowahi kutamba Real Madrid ya Hispania, maarufu kama Real Madird Legends ambao watazuru nchini mwezi ujao.
    Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Madrid watakuja nchini Agosti 22.
    Wanakuja bongo; Roberto Carlos, Ronaldo Lima, Luis Figo na Zinadine Zidane wanatarajiwa kuzuru na kikosi cha magwiji wa Real Madrid nchini mwezi ujao 

    Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
    Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah na Meneja ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema; “kila kitu  safi”.
    Ssebo ameiambia BIN ZUBEIRY leo mjini Dar es Salaam kwamba, kesho watakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari, Saa 4:00 asubuhi katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam kutaja wadhamini wa ziara hiyo.
    “Tutazungumza na Waandishi wa Habari kesho, kutaja makampuni ambayo hadi sasa yamejitokeza kudhamini ziara hii,”amesema Ssebo ambaye pia ameongeza; “Kwa ujumla maandalizi yote yanaendelea vizuri,”.
    Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.
    Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUMEKUCHA ZIARA YA REAL MADRID NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top