• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  RASMI, OSPINA ALIYETISHA KOMBE LA DUNIA ATUA ARSENAL

  KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili wa kipa wa Nice, David Ospina kwa dau la Pauni Milioni 3.2, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo ya Ufaransa, Claude Puel.
  Ospina aliivutia The Gunners kufuatia kuranya vizuri akiidakia Colombia katika Kombe la Dunia hadi kuifikisha Robo Fainali, ambako walitolewa na wenyeji, Brazil.
  Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiunga na timu hiyo ya Kaskaizni mwa London kwa mkataba wa miaka minne. Puel amezungumzia habari za kuondoka kwa Ospina alipohojiwa na Sky Sports na kusema: "Imethibitishwa, ndiyo. Akiwa na umri wa miaka 25 ni muhimu kwake kupata uzoefu wa mashindano mengine, hivyo ni uhamisho mzuri wake,".

  Kipa mpya: David Ospina aliisaidia Colombia kufika Robo Fainali katika Kombe la Dunia kabla ya kutolewa na Brazil
  Colombian connection: David Ospina
  Pole position: Wojciech Szczesny
  Uwezo utamuweka mtu langoni: David Ospina (kushoto) atagombea mamba na kipa wa sasa wa kwanza wa Arsenal, Wojciech Szczesny

  Inafahamika kwa sasa kipa huyo anakwenda kuchukua nafasi ya Lukasz Fabianski, ambaye amejiunga na Swansea, kwenda kuwa wa pili nyuma ya kipa namba moja wa sasa wa klabu hiyo, Wojciech Szczesny.
  Pamoja na hayo, kocha Arsene Wenger amesema uwezo ndio utakaomfanya mmoja wao awe kipa mamba moja wa klabu, huku Ospina akionekana kabisa kuitaka kuwa chaguo la kwanza.
  "Unajua mwanzoni Szczensy atakuwa mamba moja, kisha tena uwezo wa mtu ndiyo utaamua, ikiwa Ospina ataonyesha ni bora, atacheza,"aliiambia ESPN.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RASMI, OSPINA ALIYETISHA KOMBE LA DUNIA ATUA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top