• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 25, 2014

  MASHUJAA KUPIGA ‘TOUR’ NCHI NZIMA

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  BENDI muziki ya mashujaa 'Wana Kibega' inafanya ziara ya nchi nzima, ikiwa kushukuru wapenzi wake kwa kuwa bendi bora ya mwaka, pamoja na kupata udhamini kutoka kampuni ya vinywaji ya Bavaria.
  Mkurugenzi wa mawasiliano wa bendi ya Maxmilian Luhanga, alisema kuwa ziara hiyo itaanza jumapili mara muonekano wa mwezi, kutokana na onesho lake la kwanza kuanza siku ya Idd mosi.
  Luhanga alisema onesho hayo ni maombi ya wapenzi wa bendi, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kuwapigia kura na kushinda, katika tuzo za muziki kwa bendi yao kuwa bendi bora ya mwaka.
  Alisema kuwa ni vizuri kupita kwa wadau wao na kuwashukuru kwa kujitolea kuwapigia kura na kushinda tena kama ilivyokuwa mwaka jana.
  Pia Luhanga alisema bendi hiyo imepata udhamini wa ziara nzima kutoka kwa kampuni ya Bavaria, ambapo hata magari yao, wanayotumia yamewekwa  lebo ya kinywaji hicho.
  "Tunashukuru bavaria wameamua kutupa udhamini ambao utasaidia hata katika ziara yetu, hii ya kutembea nchi nzima, tunaomba wapenzi mtupokee kwa wingi katikasehemu tutakazofanya maonesho yetu"alisema Luhanga.
  Alisema kuwa onesho lake la kwanza litakuwa kati ya Julai 28 au 29, kwenye ukumbi wa Makonde Beach uliopo Mkoani Mtwara, onesho la pili litafanyika kwenye Ukumbi wa Emirate Hall, Masasi.
  Alisema kuwa Julai 30, watakuwa kwenye Ukumbi wa Nachingwe Resort, na Julai 31, watakuwa kwenye Ukumbi wa Mbinga Resort.
  Agosti mosi bendi hiyo itakuwa ndani mji wa Songea, ambapo itafanya onesho lake kwenye Ukumbi wa Serengeti Pub, wakati Agosti 2, itakuwa kwenye Ukumbi maarufu wa mjini Mbeya, uitwao Mbeya City Pub.
  Luhanga alisema Agosti 3, watakuwa Mbalali Top Life, wakati Agosti 5, watamalizia ziara ya mkoani Mbeya katika Ukumbi wa Gigh Class, uliopo Tunduma, na Agosti 6, itakuwa Sumbawanga mjini ikifanya vitu vyake kwenye Ukumbi wa Mwambao.
  Alisema kuwa onesho lingine litafanyika Agosti 7,Katavi Resort, Mpanda, wakati Mkoani Kigoma, itafanya onesho lake kwenye Ykumbi wa Sandra Night Club ikiwa ni Agosti 8.
  Luhanga alisema Agosti 9, Bwalo la Maofisa wa Polisi Tabora, Mkoani Shinyanga onesho lake la kwanza litafanyika agosti 10, kwenye Ukumbi wa NSSF Hall, wakati onesho lingine litakuwa kwenye Ukumbi wa Club Ciller.
  Alisema kuwa Mkoani Kagera, litafanyika Agosti 14,. kwenye Linas Club, mjini Bukoba, onesho lingine litafanyika Mkoani Geita, Desire Club, wakati Mkoani Mwanza, onesho la kwanza litafanyika kwenye ukumbi wa Villa Park na onesho la pili Buzuruga na onesho la Mkoani Mara litafanyika kwenye Ukumbi wa Magereza Hall.
  Luhanga alisema watavuka mipaka wataenda nchini Kenya, ambapo wataanza Agosti 20 mpaka Agosti 24, mara baada ya maonesho hayo, wataenda Mkoani Tanga, ambapo agosti 28 na 29, watakuwa mkoani Tanga, Agosti 30 watakuwepo Arusha.
  Mkoani mengine ambayo mashujaa 
  itafanya onesho lake ni Singida,ambapo itakuwa Agosti 31, wakati Mkoani  Dodoma, itakuwa Septemba 5 na Morogoro itakuwa Septemba 7.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHUJAA KUPIGA ‘TOUR’ NCHI NZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top