• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 23, 2014

  DILI LA BALOTELLI KUTUA ARSENAL LAFA KIFO CHA KAWAIDA, INZAGHI ASEMA ANAMPA NAFASI NYINGINE KIJANA AC MILAN

  KOCHA mpya wa New AC Milan, Pippo Inzaghi amesema a tampa nafasi nyingine mshambuliaji Mario Balotelli kudhihirisha umuhimu wake katika timu- maana yake mpango wa kuhamia Arsenal umekufa kifo cha kawaida.
  Inzaghi aliichezea mechi zaidi ya 200 The Rossoneri, akishinda nato mataji mawili ya livi na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na baada ya uongozi wa klabu kumchoka Balotelli kiasi cha kutaka kumuuza, mkongwe huyo ameweka wazi anampa nafasi tena.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 40 amesemad: "Balotelli ni mchezaji muhimu sana na mali ya Milan. Nitamchukulia yeye kama ninavyowachukulia wachezaji wengine,"amesema.

  Mazoezi makali: Mario Balotelli akijifua gym na AC Milan

  "Nitasahau kila kitu nilichosikia kuhusu yeye kiwi kibaya au kizuri, kwa sababu nataka kuwajua watu ili kupata undani wao,".amesema kocha huyo ambaye yupo Marekani na kikosi chake kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Inzaghi amechukua nafasi ya mchezaji menzake wa zamani, Clarence Seedorf kuikochi Milan lakini tayari ameweka wazi namna ambavyo Balotelli anafaa katika mipango yake.
  Selfie: Inzaghi poses for photos with a fan in New York
  Inzaghi akiwa na shabiki mjini New York
  Posers: Keisuke Honda with teammates Sulley Muntari and Mario Balotelli
  Balotelli akiwa na Keisuke Honda Sulley Muntari 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DILI LA BALOTELLI KUTUA ARSENAL LAFA KIFO CHA KAWAIDA, INZAGHI ASEMA ANAMPA NAFASI NYINGINE KIJANA AC MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top