• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 31, 2014

  LIVERPOOL YAITANDIKA MAN CITY 3-1 MAREKANI...YAYA TOURE AKOSA PENALTI

  LIVERPOOL imaifunga kwa penalti 3-1 Manchester City kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 katika mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya Uwanja wa Yankee, Marekani. 
  Man City ilipata mabao yake kupitia kwa Stevan Jovetic dakika za 53 na 67 wakati mabao ya Liverpool yalifungwa na kwa Jordan Henderson dakika ya 59 na Raheem Sterling dakika ya 85.
  Mikwaju ya penalti ya Yaya Toure na Jesus Navas iliokolewa na Mignolet wakati pia Aleksandar Kolarov naye alikosa kwa kupaisha- hivyo kumpa nafasi Lucas Leiva kuipa ushindi wa 3-1 timu ya Brendan Rodgers. Iheanacho pekee aliifungia City. 
  Sturridge pia alipaisha penalti yake, lakini Emre Can na Henderson walifunga kabla ya Lucas kutumbukiza kambani ya ushindi.
  Timu hiyo ya Merseysiders sasa itamenyana na AC Milan mjini Charlotte Jumamosi ikiwa na nafasi ya kuongoza kundi lake- ili ikutane na mahasimu, Manchester United inayofundishwa na Louis van Gaal mjini Miami.

  Shughuli ya kiumeni: Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge akipambana na klabu yake ya zamani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAITANDIKA MAN CITY 3-1 MAREKANI...YAYA TOURE AKOSA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top