• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 25, 2014

  KIDUNDA APANDA ULINGONI LEO NDONDI ZA JUMUIYA YA MADOLA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  BONDIA wa Tanzania, Selemani Kidunda anapanda ulingoni leo katika Michezo ya Jumuiya ya Madola nchini Scotland kuzipiga na Mnigeria, Kehinde Ademuyiyiwa kuanzia Saa 1:45 usiku katika pambano la uzito wa Kg69.
  Mabondia wote walipima uzito na afya jana kuanzia Saa 2:00 hadi Saa 4:00 asubuhi kwa saa za Scotland na michuano ya ndondi itaanza leo hadi Agosti 2 katika ukumbi wa Secc (Hall 4A), Nahodha wa Tanzania, Selemani Kidunda akianza kupeperusha bendera ya taifa.
  Selemani Kidunda akiwa rais Jakaya Kikwete. Nahodha wa Tanzania anapanda ulingoni leo Scotland


  Kesho Saa 7:20 mchana Nasser Mafuru atazipiga na bondia wa Ghana, Jessie Lartey katika pambano la Kg60, wakati baadaye Fabian Gaudence atazipiga na Steven Thanki wa Malawi.
  Julai 27, Saa 12:45 jioni Ezra Paul wa Tanzania atazipiga na Bye kabla ya Saa 1:40 usiku Mohamed Hakimu wa Tanzania pia kuzipiga na Sumit Sangwan wa India.
  Julai 28 Saa 7:25 mchana, Emilian Patrick atazipiga na Bashiri Nasir wa Uganda kabla ya Hemed Furahisha kupanda ulingoni Saa 1:35 jioni kuzipiga na Paddy Barnes wa Ireland ya Kaskazini.

  RATIBA YA MABONDIA WA TANZANIA JUMUIYA YA MADOLA

  Julai 25, 2014: 
  Selemani Kidunda Vs Kehinde Ademuyiyiwa (Nigeria) Saa 1:45 usiku  Kg69
  Julai 26, 2014:
  Nasser Maffuru Vs Jessie Lartey (Ghana) Saa 7:20 mchana Kg60
  Fabian Gaudence Vs Steven Thanki (Malawi) Saa 1:00 usiku Kg64
  Julai 27, 2014:
  Ezra Paul Vs Bye Saa 12:45 jioni Kg52
  Mohamed Hakimu Vs Sumit Sangwan (India) Saa 1:40 jioni Kg8I
  Julai 28, 2014: 
  Emilian Patrick Vs Bashiri Nasir (Uganda) Saa 7:25 mchana Kg56
  Hamed Furahisha Vs Paddy Barnes (Ireland Kaskazini) Saa 1:35 jioni Kg49
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIDUNDA APANDA ULINGONI LEO NDONDI ZA JUMUIYA YA MADOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top