• HABARI MPYA

    Sunday, July 20, 2014

    KOZI YA UKOCHA LESENI A SASA KUFANYIKA AGOSTI

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    KOZI ya ukocha wa mpira wa miguu ya leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyokuwa ianze kesho (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa itafanyika mwezi ujao.
    Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na maelekezo ya CAF ambayo ndiyo itakayosimamia na kuendesha kozi hiyo itakayoshirikisha makocha wenye leseni B za shirikisho hilo.
    Tarehe rasmi ya kuanza kozi hiyo itatangazwa wiki ijayo.
    Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola ana nia ya kujiendeleza zaidi
    Mwezi uliopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na CAF liliendehsa kozi ya leseni B iliyoshirikisha makocha 29 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOZI YA UKOCHA LESENI A SASA KUFANYIKA AGOSTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top