• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 22, 2014

  WABONGO HAOO NDANI YA CAMP NOU, BARCELONA...MAMBO YA CASTLE LAGER

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WANYWAJI wanne wa Castle Lager wamejishindia safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda kutembelea Uwanja wa Camp Nou wa FC Barcelona baada ya kuibuka washindi katika kampeni ya Kombe la Dunia ya Castle Lager iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Castle Lager ilikuwa mdhamini wa matangazo ya luninga ya Kombe la Dunia kupitia kituo maarufu barani Afrika cha SuperSport na kampeni hii ilienda sambamba na udhamini huu.

  Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo akionyesha coupon za washindi wanne waliobahatika kushinda safari ya kwenda kutembelea uwanja wa Camp Nou wa FC Barcelona nchini Hispania kushuhudia timu hiyo ikicheza na kuonana na wachezaji wa timu hiyo wakati wa droo kubwa iliyoendeshwa na Castle Lager sambamba na udhamini wake kwa matangazo ya televisheni ya kombe la dunia.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye droo hiyo kubwa ambapo pia washindi walitangazwa, Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo alisema kwamba promosheni zilifanyika nchi nzima kila siku ya mechi ambapo Castle Lager iliwaletea wanywaji wake matangazo ya mpira moja kwa moja kutoka Brazil kwa kuonyesha mechi zote bure kupitia bar mbalimbali nchini.
  “Mbali na kuonyesha mechi moja kwa moja, Castle Lager ilitoa manufaa mengine ya ziada kwa wanywaji na wapenzi wa soka. Kupitia promosheni mbalimbali, wanywaji walipata nafasi ya kujishindia safari ya kwenda Camp Nou huko Hispania na kukutana na baadhi ya wachezaji wa FC Barcelona walioshiriki kwenye kombe la dunia mwaka huu”
  “Maeneo ambayo tuliweza kuonyesha mechi hizo ni mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Mwanza, Kahama na Shinyanga. Wanywaji walikuwa wakijishindia zawadi mbalimbali za papo hapo na kuingia kwenye droo kubwa ambayo tumeifanya leo na kupata washindi wane watakaoenda Camp Nou na washindi wawili wamejishindia jezi zilizosainiwana wachezaji wa FC Barcelona”
  Meneja wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo na Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Majid wakichanganya tiketi za bahati nasibu ya kwenda Camp Nou Barcelona kwenye droo kubwa iliyoendeshwa na Castle Lager sambamba na udhamini wake kwa matangazo ya televisheni ya kombe la dunia. 

  Nshimo alisema kwamba walioshinda safari ya kwenda Camp Nou Hispania ni Theodore Kalugendo wa Mwanza, Peter Namika wa Morogoro, Joyce Mcharo wa Dar es salaam na Hamidu Ponza wa Dar es salaam huku waliojishindia jezi zilizosainiwa na wachezaji wa FC Barcelona ni Rebecca Nyenza na Shukuru Kitime wa Iringa.
  “CASTLE Lager siku zote inajitahidi kuwaletea na kuwapa burudani wanywaji wake na wapenzi wa soka nah ii ni mojawapo ya mambo tunayofanya kuonyesha jinsi tunavyowathamini wanywaji wa Castle Lager kwa kutuunga mkono na wakati huo huo tukihakikisha nao wananufaika na ushirikiano wetu na FC Barcelona kwa kutoa nafasi hii ya kipekee kwenda Camp Nou na kukutana na wachezaji maarufu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanaoichezea club hiyo maarufu zaidi duniani.” Alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WABONGO HAOO NDANI YA CAMP NOU, BARCELONA...MAMBO YA CASTLE LAGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top