• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 27, 2014

  VAN GAAL AENDELEZA WIMBI LA USHINDI MAN UNITED...ROONEY MOTO CHINI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Wayne Rooney amemdhihirishia ubora wake kocha mpya wa Manchester United, Mholanzi Louis van Gaal usiku huu baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya AS Roma mjini Denver, Marekani. 
  Katika mchezo wa kujianda na msimu, Rooney alifunga katika dakika za 36 na 44 kwa penalti, wakati bao lingine la United lilifungwa na Juan Mata dakika ya 39.
  Mabao ya Roma yalifungwa Miralem Pjanic dakika ya 75 na mkongwe Francesco Totti kwa penalti dakika ya 88.

  Anatisha: Rooney akishangilia na wenzake, Antonio Valencia na Ander Herrera baada ya kufunga bao la kwanza
  Opener: Rooney opened the scoring for United with a sublime strike from 25 yards in Denver
  La kwanza: Rooney alifunga bao la kwanza kutoka umbali wa mita 25 mjini Denver
  On form: Juan Mata scored with a superb lob as the first-half came to a close
  Yuko vizuri: Juan Mata alifunga bonge la bao kipindi cha kwanza

  Mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Allen Chapman mbele ya mashabiki 54,117, Rooney aliibuka mchezaji bora baada ya filimbi ya mwisho.
  Kikosi cha Manchester United kilikuwa; Johnstone/Amos dk45, Blackett, Jones/M Keane dk45, Evans/Smalling dk45, Valencia/Young dk45, Herrera/Nani dk45, Cleverley/Hernandez dk69, Mata/Kagawa dk45, James/Shaw dk45, Rooney/W Keane dk45 na Welbeck/Lingard dk45.
  AS Roma; Skorupski, Calabresi/Somma dk45, Benatia, Romangnoli/Castan dk45, Emanuelson/Cole dk45, Ucan, Keita/Pjanic dk68, Iturbe/Ljajic dk45, Paredes/Nainggolan dk45, Florenzi/Totti dk6 na Destro
  Spot: Rooney scored his second and United's third from the penalty spot as his side ran riot before the break
  Tuta: Rooney akifunga kwa penalti
  Mine: Rooney stretches in an attempt to get the ball from Mattia Destro
  Rooney akigombea mpira na Mattia Destro
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VAN GAAL AENDELEZA WIMBI LA USHINDI MAN UNITED...ROONEY MOTO CHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top