• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 22, 2014

  BOJAN AMKIMBIA SUAREZ BARCELONA, AJITIA KITANZI MIAKA MINNE STOKE CITY

  KOCHA wa Stoke City, Mark Hughes amekamilisha usajili wa mchezaji wa tano kuelekea msimu ujao, baada ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona, Bojan Krkic kwa mkataba wa miaka minne.
  Bojan – ambaye awali alimvutia Hughes alipokuwa kocha wa Manchester City miaka mitano iliyopita– amekamilisha uhamisho wake kutua The Potteries leo mchana baada ya kukiri kusajiliwa kwa Luis Suarez Nou Camp kunazidi kupunguza nafasi yake ya kucheza La Liga.
  Taarifa katika akaunti ya Twitter ya Stoke imesema: 'HolaBojan Stoke City inayo furaha kuthibitisha usajili @BoKrkic kutoka @FCBarcelona kwa mkataba wa miaka 4'.

  Krkic (kulia) angesotea namba kama angebaki Barcelona 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOJAN AMKIMBIA SUAREZ BARCELONA, AJITIA KITANZI MIAKA MINNE STOKE CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top