• HABARI MPYA

    Monday, July 21, 2014

    MISS KANDA YA MASHARIKI AGOSTI 8

    Na Samira Said, DAR ES SALAAM
    SHINDANO la urembo la kumpata malkia wa Kanda ya Mashariki limepangwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu kwenye Ukumbi wa hoteli ya Nashera
    iliyoko mkoani Morogoro.
    Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo, Alex Nikitas, alisema kuwa warembo 14 ndio watachuana kuwania taji la kanda hiyo.
    Nikitas alisema kuwa shindano hilo litashirikisha warembo kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na wenyeji Morogoro.  Aliongeza kuwa maandalizi ya shindano hilo yako katika hatua za mwisho
    Miss Kanda ya Mashariki mwaka jana Diana Laizer

    na washiriki wanatarajia kuingia kambini mapema wiki ijayo kujiandaa na kinyang'anyiro hicho.
    "Mwaka huu tumejipanga kufanya shindano lenye ubora wa hali ya juu, tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kujitokeza kushuhudia fainali za kanda hii ambayo safari ya mshindi wa taifa itaanzia," alitamba mratibu huyo.
    Alisema kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu watapata nafasi ya kuiwakilisha kanda hiyo katika fainali za Taifa "Redd's Miss Tanzania 2014" zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu.
    Diana Laizer kutoka Morogoro ndiye mrembo anayeshikilia taji la kanda hiyo ya Mashariki na katika fainali zilizopita za Redd's Miss Tanzania
    alifanikiwa kuingia katika hatua ya 15 bora.
    Mrembo Happiness Watimanywa wa mkoani Dodoma ndite anayeshikilia taji la taifa na mwaka huu ndiye atakwenda kuiwakilisha Tanzania katika fainali za dunia (Miss World).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MISS KANDA YA MASHARIKI AGOSTI 8 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top