• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 24, 2014

  SPURS YASAJILI WAKALI WAWILI KUIMARISHA KIKOSI, YUMO KIPA

  KLABU ya Swansea imethibitisha kumsajili Gylfi Sigurdsson kutoka Tottenham na kuwauza Ben Davies na Michel Vorm kwenda White Hart Lane, huku timu hiyo ya kusini kwa Wales ikipokea Pauni Milioni 3.5.
  Sigurdsson anarejea Swansea ambako alicheza kwa mafanikio kwa mkopo msimu wa 2012, akifunga mabao saba katika mechi 18 za ushindani alizocheza.
  Davies, mwenye umri wa miaka 21, amesaini Mkataba wa miaka mitano White Hart Lane wakati kipa Vorm, mwenye umri wa miaka 30, amesaini miaka minne.

  Kifaa kipya: Spurs imemsajili Ben Davies kutoka Swansea pamoja na kipa Michel Vorm hayupo pichani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SPURS YASAJILI WAKALI WAWILI KUIMARISHA KIKOSI, YUMO KIPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top