• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 24, 2014

  REAL MADRID YAMSAJILI ROBERTO CARLOS MPYA

  KLABU ya Real Madrid imesajili kinda la Kibrazil ambaye wanaamini atakuwa 'Roberto Carlos mpya'.
  Abner Felipe Souza de Almeida, au Abner nina linaloonekana kwenye jezi yake mgongoni, amejiunga na Real Madrid kama mchezaji huru kutoka Coritiba ya Brazil.

  Nyota inayochipua: Abner, pichani akiichezea timu ya taifa ya Brazil chini ya miaka 17 anatarajiwa kuwa beki hatari wa pembeni
  Role model: Abner will be hoping to follow in a similar path to Roberto Carlos
  Kioo chake: Abner anatumaini kufuata nyayo za Roberto Carlos

  Beki huyo wa kushoto mara moja amepewa nina 'Roberto Carlos mpya' kufuatia kutua kwake kwa vigogo hao wa La Liga. Vigogo wa Serie A, Roma walikuwa wanamtaka Abner kabla ya kuzidia kets na vigogo wenzake wa Ulaya.
  Abner atalazimika kumpiku beki mwingine wa kushoto wa Brazil, Marcelo ili kupata mamba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza Santiago Bernabeu.
  Beki huyo mwenye umri wa miaka 18 anaweza asiwe katika kiwango cha wachezaji wengine waliosajiliwa Real Madrid msimu huu, James Rodriguez na Toni Kroos - lakini anaonekana ni uwekezaji mzuri wa baadaye kwa faida ya timu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAMSAJILI ROBERTO CARLOS MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top