• HABARI MPYA

    Monday, July 14, 2014

    KHEDIRA NAYE KUTUA ARSENAL, REAL YAKUBALI PAUNI MILIONI 23 KUMUUZIA WENGER SILAHA

    KLABU ya Arsenal iko mbioni kuipiga bao Chelsea katika kuwania saini ya kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Sami Khedira kutoka Real Madrid na vyombo vya Habari Hispania zimeripoti kwamba dili la Pauni Milioni 23 tayari limekubaliwa.
    Kwa mujibu wa Sport, Khedira atasaini Mkataba wa miaka minne Emirates baada ya kugundulika kwamba Chelsea pia walikuwa wanamuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
    Mazungumzo ya Mkataba baina ya wawakilishi wa Khedira na Real Madrid yalivunjika na sasa wanajiandaa kumuuza kuliko kumuacha aondoke bure msimu ujao.

    Mshika bunduki mpya? Khedira yuko mbioni kutua Arsenal  baada ya kung'ara Brazil

    Timu ya Arsene Wenger tayari imekwishatoa Pauni Milioni 30 kumsaini mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez kutoka Barcelona, na pia iko mbioni kukamilisha usajili wa Mathieu Debuchy kutoka Newcastle.
    Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alifanya kazi na Khedira alipokuwa Real Madrid na Mreno huyo anamtaka sana kiungo huyo mkabaji, ingawa inaonekana atamkosa.
    Khedira alikosa mchezo wa Fainali Kombe la Dunia jana katakana na kuwa majeruhi, lakini bado Ujerumani ilimudu kuifunga Argentina 1-0 Uwanja wa Maracana na kutwaa taji la nne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KHEDIRA NAYE KUTUA ARSENAL, REAL YAKUBALI PAUNI MILIONI 23 KUMUUZIA WENGER SILAHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top