KIUNGO wa Ujerumani, Toni Kroos amesema anaondoka Bayern Munich na kwenda Real Madrid baada ya kuipa nchi yake Kombe la Dunia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyekuwa tegemeo la kocha Joachim Low nchini Brazil, amesema hayo jana mara tu baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Argentina katika Fainali ya Kombe la Dunia.
"Tumemaliza Kombe la Dunia vizuri mno ilivyowezekana. Sasa nakwenda Madrid, hivyo hizo ndoto mbili zimetilia,"amesema Kroos jana.
Kiungo huyo wa katikati anajiandaa kwenda kulipwa Pauni 160,000 kwa wiki Uwanja wa Bernabeu huku Bayern ikijiandaa kupokea kitita cha Pauni Milioni 20 kumuuza.
Kroos amekubali Mkataba wa miaka mitano na kikosi cha Carlo Ancelotti kinachoshikilia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.



.png)
0 comments:
Post a Comment